Jay Moe: Hip hop sio midundo/beat

Jay Moe ametoa somo juu ya muziki wa hip hop kuwa hauhusiani na beat au mdundo kama baadhi ya wasanii na mashabiki wanavyoelewa.
13329006_1599602896997920_1475641216_n
Akizungumza na Jabir Saleh aka Kuvichaka kwenye kipindi cha Ladha 3600 cha EFM, Moe alisema, ” katika nguzo tano za hip hop hakuna nguzo hata moja inayozungumzia beat, ndiyo maana ni ruksa kwa msanii wa hip hop kutumia mdundo wowote ilimradi asitoke katika misingi ya hip hop.”
Jay Moe alimtolea mfano rapper Ice Prince wa Nigeria kuwa anacheza na identity ya muziki wao na anaiwakilisha game ya rap.
Ikiwa ni siku chache baada ya Jay Moe kuja tofauti na ngoma yake ya Pesa ya Madafu maswali yamekuwa mengi juu yake kutokana na kumsikia katika beat ya trap tofauti na alivyokuwa amezoeleka katika kipindi cha nyuma.
Jay Moe: Hip hop sio midundo/beat Jay Moe: Hip hop sio midundo/beat Reviewed by Unknown on 12:53 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.