Video: Diamond aweka sanamu za mafuvu ya watu ofisini kwake, Je ni ishara ya ‘kifreemasons’ ?

Ni kweli Freemasonry kama ilivyo maana yake kwanza ilkuwa ni kundi la mafundi waashi (masons) au wajenzi kuwa lugha nyingine. Walikuwa ni wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki ya zama hizo zinazoitwa kwa kizungu (medieval times).
Freem
Diamond akizungumza huku pembeni kukiwa na sanamu za fuvu za watu
Lakini miaka ya hiki karibuni kumekuwa na imani kwa watu kuwa freemasons ni imani ya kishetani ambayo imekuwa ikitumiwa na mastaa wakubwa duniani ili kufanikiwa zaidi kipesa na kuwa mashabiki wengi.
Hakuna aliyewai kuthitisha kwamba ni freemasons kama baadhi ya mitandao inavyoripoti, lakini wadau mbalimbali wa mambo duniani wamekuwa wakitoa na kuonyesha alama mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumiwa na watu hao ili kutambuana.
NEMBO-YA-FREE
Moja kati ya alama zinazodaiwa kuwa za kifreemasons
Diamond Platnumz Jumanne hii alipost video instagram akiwaeleza mashabiki wake kuhusu kuchelewa kwa kazi yake mpya ambayo ilikuwa itoke wiki iliyopita, lakini ndani ya video hiyo ambayo inaonyesha kuchukuliwa ofisini kwake, imeonyesha sanamu za mavufu mawili ya watu na kuibua maswahi mengi kwa mashabiki huwenda zikawa alama za kifremasons ambazo zimekuwa zikitumika na mastaa mbalimbali waliofanikiwa duniani.
Video: Diamond aweka sanamu za mafuvu ya watu ofisini kwake, Je ni ishara ya ‘kifreemasons’ ? Video: Diamond aweka sanamu za mafuvu ya watu ofisini kwake, Je ni ishara ya ‘kifreemasons’ ? Reviewed by Mzansi on 5:13 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.