D’banj Aunga Ndoa Kwa Siri


Staa wa muziki kutoka Nigeria, D’banj amefunga ndoa kwa siri.
Imedaiwa kuwa D’banj alifunga ndoa Jumamosi iliyopita na mchumba wake wa muda mrefu mwenye asili ya Afrika Kusini na Nigeria lakini makazi yake yapo nchini Marekani. D’banj alipost picha siku ya Jumapili ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya baba yake huku kwenye kidole chake cha mkono wa kushoto kikiwa kimevalishwa pete ya ndoa.
Mwezi April D’banj alipohojiwa na Premium Times, alisema, “Who said I am not married? I would tell you the truth, I am not married but if I am, nobody would hear about it. It is going to be a very quiet wedding.”
Taarifa za ndani zimedai kuwa harusi hiyo ilihudhuriwa na watu wachache zaidi wakiwemo wazazi wa msanii huyo pamoja na watu wake wa karibu tu.
D’banj Aunga Ndoa Kwa Siri D’banj Aunga Ndoa Kwa Siri Reviewed by Mzansi on 5:05 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.