Audio: Shilole Ageuka Mbogo Hewani Alipoulizwa Maswali ya Jike Shupa na Nuh Mziwanda

Mtangazaji wa Kings FM, Divine Kweka alijikuta akitamani akate simu na aingie chini ya uvungu baada ya maswali yake kumpanikisha Shilole.

Mtangazaji huyo alianza vizuri mahojiano yao kwa kumuuliza kuhusu wimbo wake na Barnaba ‘Say My Name’ kabla ya mambo kugeuka alipomuuliza kuhusu Nuh Mziwanda na model wa Jike Shupa, Zuu.

“Siwezi kuzungumzia hiyo kitu sababu hainihusu,” alijibu Shishi baada ya kuulizwa anachukuliaje makavu anayopewa na ex wake.

“Sihitaji kuongelea hivyo vitu, niulize kuhusiana na muziki wangu, mambo yangu yanavyoenda, usiniulizie vitu vya watu ambao siwajui mimi,” alifoka muimbaji huyo.

Kwa upande mwingine Shilole amedai kuwa anakuja na ngoma aliyoipa jina ‘Hatutoi Kiki.’

Msikilize zaidi hapo chini. 
Audio: Shilole Ageuka Mbogo Hewani Alipoulizwa Maswali ya Jike Shupa na Nuh Mziwanda Audio: Shilole Ageuka Mbogo Hewani Alipoulizwa Maswali ya Jike Shupa na Nuh Mziwanda Reviewed by Goodluck Mathias on 5:17 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.