Msanii
wa muziki kutoka Tip Top Connection Madee Ali amesema kama angekuwa
anatumia Madawa ya kulevya na tayari ameshaathirika basi angewataja wale
wanaomuuzia ili kuisaidia serikali kutokomeza matumizi ya madawa ya
kulevya.
Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television, Madee amesema serikali inaweza kutokomeza biashara ya Madawa ya kulevya kama ikiwatumia wale walioathirika.
“Ningekuwa mimi natumia Madawa ya kulevya na tayari yameshaanza kuniathiri si utaulizwa imekuwaje kuwaje, nani amekufundisha hizi mambo, umeanza wapi umenunua kwa nani, ina maana nitaanza kumtaja yule ambaye ameniuzia, na ambaye ameniuzia mimi kikete, yeye atamtaja bosi wake, bosi wake atamtaja yule bosi wake mkubwa kwa hiyo ile cheni yote itakuja mpaka itamfikia yule kigogo anayeingiza kutoka nje”, alisema Madee
Pia Madee alisema ingawa wasanii wana nafasi yao katika kupambana na biashara ya Madawa ya kulevya, lakini serikali ndio chombo ambacho kinaweza kupambana na biashara hiyo na inatokomeza kabisa.
BY: MOHAMMED KITALAMBO

Madee: Ningekuwa Nimeathirika na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, Ningewataja Wanaoniuzia
Reviewed by Unknown
on
12:58 PM
Rating:
Reviewed by Unknown
on
12:58 PM
Rating:

No comments: