Muhimbili Kuna Kitengo cha Kuhudumia Mashoga..Shoga Maarufu Afunguka Kupitia Take One ya Zamaradi

Hii nimeisikia jana kupitia kijana mmoja shoga aliyekuwa akihojiwa katika kipindi kimoja kwenye tv. Alijiweka bayana sana na hakuficha jambo, kitu kilichonistaajabisha kwa uwazi wake. Hata changudoa si rahisi kujianika kiasi kile.

Akasema Muhimbili wana kitengo chao cha kuhudumiwa. Kwamba hupewa mafuta ya ky, kondom, sabuni, hasa za kusafishia kinywa baada ya blow job, n.k. Hiki kitengo mbona kipo katika taasisi nyeti kiasi hiki? Serikali waliridhia vipi kuweko kwa kitengo hiki pale? Ni nani wafadhili?

Mbona huwa hatusikii kikitangazwa kama vitengo vingine vya waathirika wa ukimwi na madawa ya kulevya? Kwa huu unyeti wake na aina ya huduma wanazotoa hapo ni wazi kwamba ushoga si jambo jema kabisa. Kwamba ushoga ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine tajwa hapo juu.

Lakini kinachonishangaza kuhusu huu ugonjwa wa ushoga, mbona wanawapa vitendea kazi kama mafuta na kondom kuliko kuwaelimisha waache ushoga?

Kingine nilichobaini ni kuwa ushoga huooooo umeanza kuchomoza hadharani na kwa staili yake. Baada ya miaka mitano tutauona ushoga ni jambo la kawaida nchini kama hali ikiachwa hivi.

Nimalizie tu kwa kumnukuu huyo shoga aliposema, mboga saba... ya nane pilipili. Yaani mtoto wa kiume asidekezwe sana na wazazi kwani kufanya hivyo kutamuingiza katika majanga kama vile ushoga. Hiyo ni tafsiri yangu
Muhimbili Kuna Kitengo cha Kuhudumia Mashoga..Shoga Maarufu Afunguka Kupitia Take One ya Zamaradi Muhimbili Kuna Kitengo cha Kuhudumia Mashoga..Shoga Maarufu Afunguka Kupitia Take One ya Zamaradi Reviewed by Unknown on 3:28 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.